DAR ES SALAAM – Baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa wamejumuika na familia kupokea mwili wa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Marehemu Dk Faustine Ndugulile baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na kisha kuupeleka katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.