RUVUMA; RAIS Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 27, 2024 amezindua Shule ya Wasichana ya mchepuo wa Sayansi na Sanaa ya Dk Samia Suluhu Hassan, iliyopo katika kitongoji cha Migeregere, Kata ya Rwinga, Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,200 na mpaka sasa wanafunzi waliopo ni 548.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule 26 za wasichana za sayansi za mikoa zilizojengwa kwenye Mikoa yote Tanzania Bara na imejengwa kwa gharama ya shilingi Bil. 4.6, ikiwa vyumba vya madarasa 22, mabweni 8, nyumba za walimu 3 (2 kwa 1), Nyumba ya Mkuu wa shule, nyumba ya Matron, chumba cha TEHAMA, maktaba, jengo la utawala pamoja na uzio upande wa mabweni.