Pinda ataka mfumo bora ukusanyaji tafiti za kilimo

ARUSHA: WAZIRI Mkuu Mstaafu ,Mizengo Pinda ameagiza kuanzishwa mfumo maalumu wa ukusanyaji tafiti zinazofanywa na wataalamu wa kilimo ili kuiwezesha serikali kuzifanyia kazi na kubaini changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na uongezaji tija katika kilimo.

Aidha, katika kuhakikisha utafiti unakua na tija serikali imeimarisha utafiti kwa kutenga Sh bilioni 40.73 kwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kwa ajili ya uzalishaji wa teknolojia mpya 64 zinazoongeza ufanisi na ustahimilivu wa uzalishaji.

Pinda amesema hayo wakati wa ufunguzi mkutano wa  nne wa  mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Sayansi za Mazao (CROSAT)na kujadili namna ya kuendeleza uzalishaji wa mazao unaostahimili mabadiliko ya tabianchi unayofanyika jijini Arusha na kukutanisha wakulima, wauzaji wa pembejeo za kilimo, watafiti na wadau mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA).

Amesema endapo tafiti hizo zikiingizwa katika mfumo maalumu zitawezesha serikali kubaini changamoto za wakulima ni zipi katika kila mkoa na kuzifanyia kazi ili kuwezesha sekta ya kilimo kuongeza ajira zaidi pamoja na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo.

“Asilimia 65.6 ya watanzania wanajihusisha na masuala ya kilimo huku upande wa mazao sekta hiyo  imekua kwa asilimia 4.2 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 2.7 mwaka 2022 ambapo mchango katika Pato la Taifa uliongezeka hadi asilimia16. 1”

Amesema serikali itaendelea kuhakikisha Mpango a Kesho iliyobora (BBT) unawafikia zaidi vijana maeneo waliyopo ili kuleta matokeo bora ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 na Mpango Kabambe wa Mageuzi ya Sekta ya Kilimo katika nyanja mbalimbali za kisera,kiuchumi na uwezeshaji

Huku, Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Sayansi za Mazao (CROSAT) Profesa, Kalunde Sibuga amesema chama hicho kinajumla ya wanachama 294 kutoka sekta binafsi, mashirika na wataalam mbalimbali na kusisitiza ji vema salsa wataalam hao kushirikiana na serikali katika kuhakikisha sekta ya kilimo inakua na kuwezesha ajira katika kada mbalimbali kwakutumia teknolojia za kisasa ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button