Pochettino asaini Chelsea

RASMI Mauricio Pochettino amesaini mkataba wa kuifundisha Chelsea, makubaliano baina ya pande hizo mbili yalifanyika wiki mbili zilizopita. Mwandishi wa habari za michezo Fabrizio Romano amethibitisha.

Taarifa ya Romano imeeleza kuwa Chelsea watamtangaza Pochettino muda wowote kuanzia sasa kuwa kocha mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kocha huyo wa zamani wa Spurs ataanza kazi wiki ijayo baada ya leo kuhitimishwa msimu wa Ligi Kuu England. Lampard ataondoka rasmi baada ya mchezo wa leo dhidi ya Newcastle United

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button