Polisi wavamia ofisi ya Rais Yoon Suk

KOREA KUSINI : POLISI nchini Korea Kusini wamevamia ofisi ya rais mjini Seoul, kufuatia jaribio la Rais Yoon Suk Yeol la kutaka kutangaza sheria ya kijeshi wiki iliyopita.
 
Wataalam wa siasa wamedai kuwa uvamizi huo uliofanywa na polisi nchini humo ni mgumu sana kufanyika katika siasa za Korea Kusini.
 
Rais Yoon, ambaye amesalia madarakani licha ya kura ya kumuondoa madarakani kumtaka ajiuzulu, anakabiliwa na uchunguzi kadhaa kutoka vitengo mbalimbali vya serikali, kwa mashtaka ya uasi na uhaini.
 
Wakati huo huo, waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo Kim Yong-hyun alifanya jaribio la kutaka kujiua wakati akiwa kizuizini Jumanne usiku. SOMA:  Rais Yoon Suk atangaza hali ya hatari
 
Hatahivyo, maafisa wa karibu na Rais Yoon Suk wamejiuzulu kufuatia tangazo la sheria ya kijeshi.