Polisi yakemea propaganda ajali mgodi Msasa -Geita

JESHI la Polisi mkoani Geita limewatahadharisha wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Msasa wilayani Bukombe mkoani Geita kuepuka propaganda za uchochezi wa uvunjifu wa amani.
Kauli ya Jeshi la Polisi inakuja kufuatia kusambaa wa taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii juu ya athari za ajali ya kuporomoka kwa maduara(mashimo) manne katika mgodi huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa mgodi huo kufuatia ajali iliyotokea Machi 29, 2025 mgodini hapo.
Kamanda Jongo amesema vyombo vya usalama vimechukua hatua stahiki kufuatilia kwa kina kama kuna miili ya watu katika eneo lilititia na hadi Machi 30, 2025 hakuna mwili uliopatikana.
Amesema wachimbaji wadogo na watanzania wote wanapaswa kuachana na propaganda zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna ifdadi kubwa ya watu wamefariki dunia.

Amesema watu wachache wasiolitakia mema taifa ndio wamekuwa vinara wa kusambaza taarifa hizo jambo ambalo halipaswi kuungwa mkoano kwa maslahi mapana ya taifa.
Kamanda Jongo ametumia mkutano huo kuwahoji wananchi na wachimbaji iwapo kuna mwenye taarifa za ndugu au mfanyakazi mwenza ambaye hajaonekana tangu kutokea kwa hitilafu hiyo.
Amethibitisha kuwa baada ya mazungumzo na wananchi waliohojiwa katika eneo hilo nao wamekiri kwa pamoja kuwa hakuna mtu aliyekosekana wala kupata madhara kutokana na tukio hilo.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa jitihada zetu za ufukuaji zimethibitisha kuwa hakuna aliyepata madhara.
“Tunapaswa kuwa makini na taarifa zisizo rasmi zinazoeneza hofu. Kitaalamu tumefanya kila linalowezekana kujiridhisha na usalama wa eneo hili,” amesisitiza Kamanda Jongo.

Kaimu Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, ASF Keneth Mwakasitu, amewahakikishia wananchi kuwa timu za uokoaji zipo eneo la tukio na zimefanya kazi kwa umakini mkubwa.
ASF Mwakasitu amewataka wachimbaji wadogo na watanzania wote kwa ujumla kuwa na Imani na jeshi la zimamoto na uokoaji kwani dhamira yake ni kuona watanzania wote wanakuwa salama.
Ofisa Madini wa Mkoa wa Kimadini Mbogwe, Joseph Mrimi, amesema hatua stahiki za uchunguzi na ukaguzi zinaendelea kufanywa ili kudhibiti madhara mengine katika mgodi huo wa Msasa.




I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do…… http://www.giftpay7.vip
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com