Polisi yatangaza operesheni kamata mifugo

Jeshio la Polisi latangaza operesheni kamata mifugo| TanPol

JESHI la Polisi Kupitia kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wafugaji na wakulima limesma kuanzia leo September 18 litaendesha operesheni kali nchi nzima kutoa elimu na kukama mifugo yote ambayo itakamatwa ikiingiaa katika maeneo yasio rasmi.

kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua ametoa kauli hiyo leo September 18 2022  alipofika katika Kijiji cha mkoga ya zamani wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya ambapo amesema katika siku za hivi karibuni kumejitokeza baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao katika maeneo ambayo sio rasimi na kuharibu mmashamba ya wakulima Pamoja na hifadhi ambazo ni urithi wa dunia.

Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua

Aidha kamanda Pasua amewataka wafugaji kufuata matumizi bora ya ardhi ili kuepuka mkono wa dora  ikiwa ni Pamoja na kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji  hapa nchini na kubainisha kuwa serikali yetu chini ya Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi imepanga maeneo kwa ajili ya ufugaji na kilimo Pamoja na uhifadhi hivyo amewataka wakulima kufuata utaratibiu uliowekwa.

Advertisement

Kwa upande wake Naibu Kamishina wa Uhifadhi wa shirika   la uhifadhi Tanzania TANAPA CC Herman Batiho amesema Zaidi ya mifugo elfu mbili imekamatwa katika hifafhi ya taifa Ruaha kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi nakubainisha kuwa operesheni hiyo inaendelea kama iliyotolewa maelekezo na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya Juma Homera.

Naibu Kamishina wa Uhifadhi wa shirika   la uhifadhi Tanzania TANAPA CC Herman Batiho

Amebainisha kuwa uhifadhi katika eneo la bonde la Ruaha ni uhifadhi muhimu kwa vyanzo vya maji katika mabwawa mbalimbali  hapa nchini ikiwemo Bwawa la mwalimu Nyerere ambalo kwa sasa linakwenda Kunufaisha  taifa, ambapo amesma wao kama wasimamizi wa rasilimali za nchi hawatofumbia macho vitendo hivyo vya baadhi ya wafugaji kuihujumu nchi.