Polisi yatawanya wabunge walioandamana ofisi ya Ruto

POLISI nchini Kenya wamewatawanya baadhi ya wabunge kutoka Muungano wa Azimio la Umoja ambao waliandamana na kuweka kambi kwenye Ofisi ya Rais, William Ruto Harambee House leo wakiitikia wito wa kiongozi wao, Raila Odinga.

Wabunge hao ni Stewart Madzayo (Seneta wa Kilifi) Enoch Wambua (Seneta wa Kitui), Robert Mbui (Mbunge wa Kathiani), Rosa Buyu (Mwakilishi wa Wanawake wa Kisumu), Edwin Sifuna (Seneta wa Nairobi), TJ Kajwang (Mbunge wa Ruaraka) wengine.

Akihutubia maafisa wa usalama katika lango la Harambee House, Seneta Sifuna alisema wataandamana hadi ofisi zingine za serikali leo kuwasilisha maombi yao.

“Tunataka tu kutoa barua hii kwa mtu sahihi. Waambie waje kuichukua.” Alisema Sifuna.

Habari Zifananazo

Back to top button