Polisi yathibitisha kuwanasa Diva, Niffer

JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la Kariakoo kwa kutumia akaunti zao binafsi kinyume na sheria na kanuni zinazoshughulikia majanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Jeshi hilo Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro aliwataja waliokamatwa kuwa ni Diva Gissele Malinzi (36) mkazi wa Mikocheni jijini Dar es salaam,na Jenifer Jovin Bilikwija (25) mkazi wa Salasala Kinondoni.

“Zilipatikana taarifa za watu wasio na mamlaka yoyote ya kisheria ya kushughulikia masuala ya majanga hasa yenye sura ya kitaifa kuanza kuchangisha pesa kwa kutumia akaunti zao binafsi suala ambalo ni kinyume na sharia,”amesema Muliro

Advertisement

Muliro amesema: “Watuhumiwa hao wanahojiwa kwa kina na jeshi la polisi linaendelea kutoa tahadhari kuwa halitasita kuchukua hatua zozote za kisheria kwa mtu au watu ambao,panapotokea matatizo,au majanga wao huona kama ni fursa ya kufanya mambo ya kujinufaisha kupitia majanga hayo.”

Muliro aliongeza kuwa: “Jeshi hilo litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zingine zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao ambao wamekamatwa.”

Muliro amesema jeshi hilo linaendelea kuhakikisha ulinzi wa eneo la ajali kwenye gorofa lililoporomoka unaimalika na hakina mtu banayeiba mali za wahanga wa ajali hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana wakati wa shughuli ya kuaga miili ya waliofariki kwenye gorofda lililoporomoka aliliagiza Jeshi la polisi kumkamata na kumuhoji mwanamitandao na mfanyabiashara, Jenifer Jovin ‘Niffer’ kwa kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na jengo la ghorofa kinyume cha sheria na kanuni.

“Tumeona kuna watu wameanza kuchangisha huko pembeni wanasema michango kwa ajili ya waathirika wa Kariakoo hapana, serikali imeendelea kupokea kutoka kwa watu wema wakileta misaada yao hapa na walichokuwa wakileta ni maji. sijaruhusu mtu yeyote huko nje aanze kuchangisha kwa ajili ya tatizo hili na hatukufanya hivyo kwa sababu kamati ya maafa ipo.”