JESHI la Polisi linawashilikia na kuwahoji kwa kina mkazi wa Mikocheni, Diva Gissele Malinzi(36), na Jenifer Jovin Bilikwija(25), mkazi wa Salasala Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kukusanya fedha kwa kutumia kwa ajili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo la ghorofa jijini Dar es Salaam Novemba 16 kwa kutumia akaunti zao binafsi.
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam SACP Muliro Muliro amesema kitendo hicho ni kinyume cha Sheria na Kanuni zinazoshughulikia majanga.
SOMA: Rais Samia aongeza muda uokoaji Kariakoo
“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam litashirikiana na Mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hawa,” amesema Muliro.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa tahadhari na halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu au watu ambao panapotokea matatizo au majanga wao huona ni fursa ya kujinufaisha.