Poltava: Urusi yakata umeme

UKRAINE : GAVANA Mkuu wa Poltava nchini Ukraine ,Filip Pronin amesema shambulizi la usiku kucha la Urusi katika eneo la kati mwa Ukraine, Poltava limeharibu miundo mbinu ya nishati na kukata umeme kwenye makazi 20.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, gavana wa eneo hilo Filip Pronin, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa hakukuwa na watu waliojetuhiwa licha ya nyumba kadhaa  zilianguka.

Katika mji wa kaskazini mashariki wa Zaporizhzhia, Gavana wa eneo hilo  Ivan Fedorov  amesema shambulizi la jana Jumatatu katika  eneo lake lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi takriban watu saba.

Advertisement

Wakati huo huo, jeshi la anga la Ukraine limesema limedungua droni 66 lakini likapoteza mwelekeo wa droni nyingine 13 kati ya 81 zilizorushwa na Urusi wakati wa shambulizi hilo la usiku kucha ambalo pia lilihusisha kurushwa kwa makombora.

SOMA : Urusi yashutumiwa hujuma za mtandao

/* */