Urusi yashutumiwa hujuma za mtandao

UJERUMANI : IDARA  ya upelelezi Ujerumani imeishutumu Urusi kuhusika na hujuma dhidi ya wanasiasa na kampuni za Ujerumani.

Kwa kushirikiana na mashirika ya kijasusi ya Marekani na washirika wengine wa kimataifa imebaini kuwa makundi yanayohusiana na idara ya ujasusi ya jeshi la Urusi GRU, yanayojulikana kwa jina la namba 29155, yamefanya hujuma za kimtandao dhidi ya jumuiya ya kujihami ya NATO na dhidi ya nchi za Umoja wa Ulaya.

Kwa mujibu wa idara ya ujasusi ya Ujerumani, makundi hayo ya Urusi yamekuwa yakifanya hujuma za kimtandao tangu mwaka 2020, kwa malengo ya kijasusi  na kuzichafua majina ya nchi  nyingine.

SOMAUrusi, Korea Kaskazini washtukiwa

Habari Zifananazo

Back to top button