Prisons, Singida Big Stars zafungiwa kusajili

Metacha Mnata

TIMU za Tanzania Prisons na Singida Big Stars zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara zimefungiwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kufanya usajili wa wachezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, hatua hiyo inataokana na timu hizo kukiuka kanuni za usajili wa wachezaji kwa kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu zingine.

“Uamuzi wa Kamati ya sheria ya Hadhi za wachezaji umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 17 (21) ya Ligi Kuu baada ya kuzikuta na kosa hilo, adhabu hiyo ni kwa dirisha moja la usajili,” ilisema taarifa hiyo.

Advertisement

Taarifa hiyo ilisema, Tanzania Prisons ilimsajili kipa Musa Mbise wa Coastal Union, wakati ikifahamu kuwa bado ana mkataba na klabu hiyo, huku Singida Big Stars ilimsainisha kipa Metacha Mnata huku mkataba wake na Polisi Tanzania ukiendelea.