WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ni muhimu kuunganisha taaluma na viwanda katika sekta ya utalii na ukarimu ili kufungamanisha maarifa ya kitaaluma na ujuzi ili kuziba pengo la wahitimu wasio na ujuzi stahiki.
Mkenda ametoa kauli hiyo jijini Arusha katika kilele cha Kongamano la Kimataifa la Kuunganisha Taaluma na Viwanda katika Sekta ya Utalii na Ukarimu.
SOMA: Wabunge wapitisha bajeti utalii
Amesema ili kufikia azma hiyo Serikali imeanzisha mfumo mpya wa elimu ya sekondari wenye mkondo wa elimu ya jumla na mkondo wa Amali ikijumuisha mafunzo ya ufundi na ufundi stadi.
Aidha Prof. Mkenda amesisitiza kuimarisha ushirikiano wa karibu kati ya vyuo na sekta ya viwanda pamoja na kudumisha ushirikiano wa kimataifa ili kuboresha sekta ya utalii na ukarimu ikiwa ni pamoja na kuzalisha wataalam mahiri kwa maendeleo ya taifa na kikanda.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania ย Jesca William amesema kongamano hilo lililoongozwa na kaulimbiu, “๐๐๐๐ป๐ด๐ฎ๐ป๐ถ๐๐ต๐ฎ ๐ง๐ฎ๐ฎ๐น๐๐บ๐ฎ ๐ป๐ฎ ๐ฉ๐ถ๐๐ฎ๐ป๐ฑ๐ฎ ๐ธ๐ฎ๐๐ถ๐ธ๐ฎ ๐ฆ๐ฒ๐ธ๐๐ฎ ๐๐ฎ ๐จ๐๐ฎ๐น๐ถ๐ถ ๐ป๐ฎ ๐จ๐ธ๐ฎ๐ฟ๐ถ๐บ๐,”litasaidia kuimarisha mafunzo katika sekta ya utalii na ukarimu pamoja na kukuza sekta hiyo.