Prof, Nombo atoa neno Taasisi ya Nelson Mandela

ARUSHA: Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa ,Caroline Nombo ameipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknlojia ya Nelson Mandela kwa kuzalisha wataalam wabobezi 213 ambao ni walimu katika vyuo vikuu mbalimbimbali nchini na kusisitiza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kuendelezwa zaidi ili kusaidia kuleta maendeleo zaidi katika tafiti,maabara za kisasa na mifumo ya undeshaji.

Pongezi hizo zimetolewa jijini Arusha wakati wa ziara ya kikazi kwenye taasisi hiyo na kujionea shughuli mbalimbimbali zinazofanyika hususan katika masuala ya tafiti na bunifu.

Amesema taasisi hiyo ni mojawapo kati ya taasisi mahiri inayotoa tafiti ikiwemo wataalamu hao wa vyuo vikuu wanaofundisha vyuo mbalimbali vilivyopo nchini.

“Shirikianeni na wataalam wabobezi katika sekta ya biashara ili muweze kutatua changamoto za ajira na kutoa fursa za ukuzaji uchumi unaotokana na tafiti za masoko ya ndani na nje ya nchi”

Naye Makamu Mkuu wa Taasisi, Profesa Maulilio Kipanyula amesema taasisi hiyo ni mojawapo ya taasisi inayotoa gunduzi za kisayansi na teknolojia ikiwemo utoaji wa matokeo ya tafiti kwa manufaa ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi ,Taaluma,Tafiti na Bunifu ,Profesa Anthony Mshandete amesema taasisi hiyo inajumla ya wanafunzi 593 pamoja na programu 33 lakini pia inafanya tafiti mbalimbali ikiwa ni maono ya kufikia malengo makubwa zaidi ya kitafiti na maendeleo katika masuala ya bunifu, tenknolojia ili kasi ya maendeleo ya tenknolojia iendane na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi zikiwemo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button