KENYA : ALIYEKUWA Waziri wa Usalama na Mambo ya Ndani ya Nchi nchini Kenya Profesa Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa Makamu wa Rais nchini Kenya.
Hafla ya kuapishwa kwa Profesa Kithure Kilindi ilifanyika hii leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta jijini Nairobi.
Prof. Kithure Kindiki anachukua nafasi ya Rigathi Gachagua aliyeondolewa madarakani hivi karibuni na Bunge la Seneti nchini humo.
Kindiki aliteuliwa na Rais wa Kenya William Ruto kuwa Makamu wa Rais lakini uteuzi wake uligubikwa na mivutano mahakamani kati ya mawakili wa serikali na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Rigathi Gachagua alifungua kesi Mahakamani kwa lengo la kuzuia uteuzi huo jambo ambalo Mahakama Kuu nchini humo imeamua kumruhusu Profesa Kithure kuwa Makamu wa Rais. .
SOMA : Gachagua aondolewa haki ya ulinzi
Mahakama Kuu nchini humo iliamua kutupilia mbali ombi la kumzuia Profesa Kithure kuapishwa kuwa Naibu Rais wa Kenya baada ya kujiridhisha kuwa hatua zote za kumuondoa aliyekuwa Makamu wa Rais Rigathi Gachagua zilifuata taratibu za kisheria.