Programu ya ‘Konekt Umeme’ yaanza Temeke

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Albert Chalamila lamezindua programu ya Konekt Umeme, Pika kwa Umeme iliyobuniwa na TANESCO katika viwanja vya Mwembe yanga wilaya ya Temeke.

Ameeleza kuwa mpango huo wa kitaifa wa Nishati umelenga kuunganisha wateja milioni 8.5 ifikapo 2030 sawa na wateja milioni 1.7 wapya kila mwaka.

Chalamila amepongeza Wizara ya Nishati, na TANESCO na wadau wote wa maendeleo kwa kuja na wazo hili bunifu lenye lengo la kuongeza upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.

Alisema programu ya Konekt Umeme, pika kwa umeme ni gharama nafuu, inaufanisi mkubwa, pia umeme unaotumika ni kidogo sana ukilinganisha na nishati zingine.

“Mpango huu ni mwanzo wa zama mpya katika historia ya huduma za umeme nchini unaounga mkono juhudi ya  Rais  Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha Tanzania na Afrika inatumia  nishati safi na  kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya umeme kupikia ambayo inaifanya jamii kwenda kwenye viwango bora vya maisha,” alisema Chalamila.

Pia Chalamila amesema ni ukweli usiopingika umeme ni hitaji muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi lakini maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa TANESCO, Lazaro Twange amesema Tanzania kupitia wizara ya Nishati, mpango huu unatoa fursa kwa mteja kupewa jiko wakati wa kuunganishiwa umeme kisha analipa kidogo kidogo kupitia mfumo wa token hivyo familia nyingi sasa zitaweza kupika kwa ufanisi na kwa gharama nafuu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button