PURA wahimizwa kuziishi tunu za mamlaka

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (kushoto pichani), Mha.

Charles Sangweni amewahimiza wafanyakazi wa PURA kuziishi Tunu za Taasisi hiyo kwani tunu hizo ni moja ya vitu muhimu vya kuzingatia ili kufikia malengo ya Taasisi.

Mkurugenzi huyo ametoa  wito huo wakati akifungua mafunzo kwa wafanyakazi wa PURA kuhusu rushwa, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukizwa yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Tunu tulizojiwekea kama Taasisi zinatutambulisha sisi ni nani, zinatengeneza taswira yetu kwa jamii, zinaathiri mitizamo yetu katika kazi na namna ambavyo tunatoa huduma zetu – kwa kutaja machache.

Hivyo, PURA haiwezi kuvumilia tabia zinazokinzana na tunu za taasisi, tabia ambazo zinakwenda kinyume na tunu hizo,” Mhandisi Sangweni amesema.

Ametumia fursa ya ufunguzi wa mafunzo kufafanua kwa undani kuhusu tunu za PURA ambazo ni uwazi, uwajibikaji, ubunifu, uadilifu na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma.

Habari Zifananazo

Back to top button