Putin akiri mapungufu vyombo vya usalama Urusi

URUSI : RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amekiri kuwa vyombo vya usalama vya nchi yake vimefanya makosa kufuatia mauaji ya Jenerali Igor Kirillov jijini Moscow, mauaji ambayo yanadaiwa kufanywa na Ukraine.

Akizungumza katika mkutano wake wa mwisho wa mwaka, Putin amesema kuwa ni muhimu kuboresha mfumo wa ulinzi wa Urusi ili kuepuka makosa makubwa zaidi.

Putin alisisitiza kuwa Urusi iko tayari kwa mazungumzo na maridhiano kuhusu mzozo wa Ukraine, lakini akaongeza kuwa inahitaji upande wa pili uwe tayari kuzungumza.
“Mimi niko tayari wakati wowote,” alisema Rais Putin.

Advertisement

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, aliahidi kufanikisha mkataba wa amani na Ukraine mara baada ya kuingia madarakani Januari.  SOMA: PUTIN – Urusi inahaki ya kutumia silaha za nyuklia

Hata hivyo, Putin amebainisha kuwa vikosi vya Urusi vinashikilia udhibiti mkubwa katika vita, ingawa hajui lini Urusi itarudisha eneo la Kursk, ambalo liliwahi kuvamiwa na Ukraine.

Kremlin pia hivi karibuni iliunga mkono ukosoaji wa Trump kwa Rais Biden kuhusu uamuzi wa kuruhusu Kyiv kutumia makombora ya Marekani kushambulia Urusi, hatua ambayo imeonekana kuongeza mzozo wa kivita ambao umeendelea kwa miaka mitatu sasa.