Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kwamba Moscow “italazimika kujibu” ikiwa Uingereza itaipatia Ukraine risasi na silaha zingine za moto zenye uranium.
Putin amezungumza hayo baada ya kusikia kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Annabel Goldie, kwamba risasi zilizokuwa na madini ya urani ni sehemu ya msaada wa kijeshi uliopelekwa Ukraine pamoja na vifaru vya vita vya Challenger 2.
“Uingereza ilitangaza sio tu usambazaji wa mizinga kwa Ukraine lakini pia makombora yenye uranium iliyopungua. Hili likitokea, Urusi italazimika kuchukua hatua,” Putin aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo na kiongozi wa China Xi Jinping katika Ikulu ya Kremlin,”
“Ikiwa haya yote yatatokea, Urusi italazimika kujibu ipasavyo, ikizingatiwa kuwa Magharibi kwa pamoja tayari imeanza kutumia silaha zenye sehemu ya nyuklia.” Alisema Putin.
Akijibu maswali kuhusu risasi hizo, Waziri Goldie alisema Jumatatu kwamba “pamoja na utoaji wetu wa kikosi cha vifaru vya Challenger 2 kwa Ukraine, tutakuwa tukitoa risasi ikiwa ni pamoja na raundi za kutoboa silaha ambazo zina uranium iliyopungua”.
Risasi hizo “zilikuwa na ufanisi mkubwa katika kushinda vifaru vya kisasa na magari ya kivita”, alisema.
Uranium iliyopungua ni zao la mchakato wa urutubishaji wa nyuklia unaotumiwa kutengeneza mafuta ya nyuklia au silaha za nyuklia. Uzito wake unaweza kutumika katika mizunguko ya kutoboa silaha kwani huwasaidia kupenya chuma kwa urahisi.
Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa umetaja risasi hizo kama “meta nzito yenye sumu ya kemikali na radiolojia”