Qatar yafikia hatua za mwisho ya mazungumzo ya Gaza

DOHA : QATAR ambayo ndio mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya kumaliza vita vya Gaza na kuwachiliwa mateka yamefikia leo hatua za mwisho na kuongeza matumaini ya kufikia makubaliano yanaendelea .

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari amesema wajumbe wamefikia sehemu ambapo masuala muhimu yaliyokuwa yakizuia muafaka kupatikana yameshughulikiwa.

“Ni muhimu sana kuzingatia tusiwape watu matarajio ambayo siyo sawa na kile kinachotokea sasa hivi. Tunaamini kuwa tumepiga hatua kubwa,” alisema Majed.

Advertisement

“Tunaamini pia tuko katika hatua za mwisho. Lakini ni wazi kwamba makubaliano hayawezi kuwa makubaliano hadi litakapotolewa tangazo rasmi kuwa yamefikiwa,” aliongeza.

“Kwa hivyo tusisherehekee kupita kiasi kwa kinachotokea sasa. Tuwe na subira, lakini bila shaka tunayo imani.” SOMA: Mjadala bado mzito Gaza

Hapo jana, Rais wa Marekani anayeondoka Joe Biden alisema mpango huo unakaribia kukamilishwa, ikiwa ni siku chache tu kabla ya kuapishwa kwa mrithi wake, Donald Trump.

Misri, Qatar na Marekani zimeimarisha juhudi za kufikiwa mpango wa usitishwaji vita ili kuwezesha kuwaachia  huru mateka wanaoshikiliwa Gaza tangu shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israel.