Rafael Nadal kustaafu mwisho wa msimu

Rafael Nadal

NYOTA wa kimataifa wa tenisi Rafael Nadal aliyeshinda mataji 22 ya Grand Slam atastaafu mchezo huo mwisho wa msimu huu.

Nadal, 28, atawakilisha Hispania katika mchezo wa mwisho wakati wa fainali za Kombe la Davis zitakazofanyika Malaga mwezi ujao.

SOMA: Nadal kukosa ‘Australia Open’

Advertisement

Nyota huyo amecheza mara chache katika misimu miwili iliyopita kwa sababu za majeraha na mwaka uliopita alitamka kwamba angestaafu mwisho wa msimu wa 2024.

Katika taarifa kwa njia ya video leo Nadal amesema: “Nipo hapa kuwafahamisha kuwa nastaafu michezo ya tenisi ya kulipwa. Ukweli ni kwamba kumekuwa na wakati mgumu miaka kadhaa, hasa miwili iliyopita.”

Mataji mengine aliyeshinda Nadal ni French Open 14, ATP 92, Masters 36 na medali ya dhahabu ya Olimpiki.

Nadal anastaafu akiwa mchezaji wa pili wa tenisi kwa wachezaji mmoja mmoja aliyefanikiwa zaidi kwa wakati wote nyuma tu ya mpinzani wake wa muda mrefu, Novak Djokovic.