CONGO : RAIA watatu wa China wamehukumiwa kifungo cha miaka 7 jela na kuamriwa kulipa faini ya dola 600,000 kwa kuchimba madini nchini Kongo kinyume cha sheria.
Washtakiwa hao pia walipatikana na hatia ya ulaghai, utakatishaji fedha na uporaji.
Raia hao walikamatwa Januari 4, wakiwa na dola 400,000 pesa taslim na vipande 10 vya dhahabu.
Mahakama ya Bukavu pia ilijumuisha kifungo cha miezi mitatu jela kwa kukaa nchini humo kinyume cha sheria. SOMA : Congo waandamana kupinga wizi wa madini
Mkoa wa Kivu Kusini una utajiri mkubwa wa dhahabu, eneo ambalo kwa kiasi kikubwa limetawaliwa na uchimbaji wa madini, huku baadhi ya migodi ikidhibitiwa na makundi ya waasi yenye kushirikiana na wafanyabiashara wasio na leseni.
Makampuni mengi ya China yanachimba dhahabu na madini mengine huko Kivu Kusini, mojawapo ya majimbo ya mashariki mwa DRC ambayo yamekumbwa na ghasia kutoka kwa makundi yenye silaha kwa takriban miongo mitatu.
Mnamo 2021, serikali ya Kongo ilisimamisha kampuni sita za uchimbaji madini za Kichina huko Kivu Kusini kwa kufanya kazi bila idhini sahihi.