MAREKANI : RAIS wa Marekani, Joe Biden yuko nchini Angola kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kukabiliana na ushawishi wa China na pia kutimiza ahadi muhimu aliyoitowa mwaka 2022 ya kuimarisha mahusiano na Bara la Afrika.
Kabla ya kuelekea nchini Angola, Rais Biden amekutana na Waziri Mkuu wa Cape Verde Ulisses Correia e Silva ambaye alifanya mazungumzo na baadaye kuelekea nchini Angola.
Nchini Angola, Rasi Joe Biden amepanga kukutana na Rais joao Lourenco wa Angola na baadaye atatembelea makumbusho ya Kitaifa ya Utumwa yaliyopo katika mji mkuu wa Luanda.
Ziara ya Biden itajikita kwenye mradi mkubwa wa reli unaounganisha bandari ya Lobito ya Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia zenye utajiri wa rasilimali.
SOMA: Museveni: Tunaweza kuendelea bila kuungwa mkono
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Marekani kuitembelea nchi ya Angola iliyokuwepo Kusini mwa Afrika yenye utajiri wa mafuta, tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1975.