PERU : MWENDESHA mashitaka mkuu wa Peru amesema ofisi yake inaanzisha uchunguzi dhidi ya Rais Dina Boluarte kwa tuhuma za kukwepa majukumu yake.
Uchunguzi huo unatokana na kuibuliwa kwa kashfa ya kiongozi huyo kutoonekana hadharani kwa muda mnamo mwezi Juni na Julai mwaka jana, akiwa kwenye matibabu ya operesheni ya pua.
Jumanne ya wiki hii,Waziri Mkuu wa zamani, Alberto Otarola, aliiambia kamati ya bunge kuwa Rais Boluarte alikwenda kufanyiwa operesheni ya pua kutokana na tatizo la kupumua.
Hatahivyo, mitandao ya kijamii nchini humo ilisambaza taarifa kuwa rais huyo alitumia muda wa kazi kufanya operesheni ya urembo wa pua .
Mbali na kashfa hiyo, Boluarte pia anakabiliwa na shutuma za kutumia wadhifa kwa mambo ya anasa na kupokea rushwa ya saa za Rolex. SOMA: Rais mstaafu Peru jela miaka 20 kisa rushwa