Rais mstaafu Peru jela miaka 20 kisa rushwa

MAHAKAMA nchini Peru imemhukumu rais wa zamani wa taifa hilo, Alejandro Toledo kifungo cha miaka 20 na miezi sita jela kwa kosa la rushwa na utakatishaji fedha haramu.

Waendesha mashtaka wanasema alichukua $35m kama hongo kutoka kwa kampuni ya ujenzi ya Brazil ambayo ilipewa kandarasi ya kujenga barabara Kusini mwa Peru.

Toledo, 78, alikuwa madarakani kuanzia 2001 na 2006.

Advertisement

Alikamatwa miaka mitano iliyopita huko California, ambako alipokuwa akifanya kazi kwa miaka mingi, na kupelekwa Peru mwaka jana.