Rais Dk Samia atoa zawadi ya krismasi Arusha

Rais Dk, Samia Hassan Suluhu ametoa zawadi za sikukuu ya krismasi kwenye vituo vitatu vya makao ya watoto Mkoani Arusha. Vituo hivyo ni Joy of God,UmuAisha na Kindeness vyote vipo Jiji la Arusha

Zawadi hizo zimekabidhiwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ambaye alisema Rais ametoa zawadi hizo ikiwa ni kuonyesha ishara ya upendo kwa watoto wanaoishi katika vituo hivyo.

Amesema Rais amekabidhi zawadi hizo ili kwaajili ya kusaidia watoto hao wenye mahitaji maalum (yatima) katika vituo hivyo ili kusheherekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya

Vitu hivyo ni biskuti boksi saba,mchele kilo 200 ,unga wa ngano kilo 200 ,mafuta Lita 90,sukari kil0100. Mkoa wa Arusha unajumla ya makao 91 yenye watoto,2,567 wakimweno wakike ni 1,291 na wanaume ni 1,276

Aidha kituo cha Joy of God kinajumla ya watoto 24,UmuAisha watoto16 na Kindness kinajumla ya watoto 45.

Naye mmoja kati ya walezi wanaokaa na watoto hao, Mohamed Ramadhani kutoka UmuAisha amemshukuru Rais kwa kutoa msaada huo kwa watoto wenye uhitaji.

Habari Zifananazo

Back to top button