Rais Guinea Bissau aunda serikali mpya
RAIS wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo ametangaza kuunda serikali mpya akiipa jukumu muhimu la kupambana na rushwa.
Kuundwa kwa serikali mpya kunakuja baada ya kuvunjwa kwa Bunge na sambamba na mapigano ya hivi karibuni ambayo Rais Embalo aliyaita jaribio la mapinduzi dhidi yake.
“Vita dhidi ya ufisadi lazima viwe msingi wa majukumu ya timu yako.
Hakuna aliye na haki ya kuchukua manufaa ya umma,” alisema Embalo,”
“Iwapo kesho tutabaini tuhuma za rushwa dhidi yako, nawe pia utafikishwa mahakamani. Taasisi zote lazima zikaguliwe. Asiwe juu ya sheria.” aliongeza.
Embalo ameteua serikali mpya yenye wanachama 33 inayoundwa na mawaziri 24 na makatibu wa serikali tisa, waliotokana na kambi yake na muungano wa upinzani wa PAI-Terra Ranka.