Rais Macron adaiwa kudhalilisha waafrika

CHAD: SERIKALI ya Chad imemshutumu Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kwa kudharau nchi za Afrika, akisema kwamba wanadhihirisha kutokushukuru licha ya msaada wa Ufaransa katika kukabiliana na uasi katika ukanda wa Sahel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Abderamane Koulamallah, alieleza kupitia taarifa iliyotolewa jana kwamba matendo ya Macron yanaonyesha jeuri na dhihaka kwa Waafrika.

Taarifa hiyo, iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa la Chad, ilisema kwamba viongozi wa Kifaransa wanapaswa kujifunza kuwa na heshima kwa Waafrika.

Advertisement

Koulamallah pia alikumbusha Ufaransa kuhusu mchango mkubwa wa Afrika, hasa Chad, katika kusaidia Ufaransa wakati wa vita vikuu vya dunia.

Waziri huyo alisisitiza kuwa mchango wa Ufaransa kwa Chad umejikita tu katika maslahi ya kimkakati ya nchi hiyo, na siyo katika maendeleo endelevu ya watu.

SOMA: Ufaransa yapigwa tena wahuni washambulia faiba