Rais Macron kulihutubia Taifa

UFARANSA: Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, anatarajiwa leo jioni kulihutubia taifa katika kipindi hiki cha kutokuwa na uhakika, huku changamoto zinazoendelea kuibuka duniani.
Hotuba ya Macron inatarajiwa wakati ambapo viongozi wa Ulaya wanatarajiwa kukutana Alhamisi kesho katika kilele cha mkutano utakaojadili ulinzi wa bara hilo na mzozo kati ya Urusi na Ukraine.
Kwa sasa, viongozi wa Ulaya wanakutana na changamoto ya kukabiliana na mabadiliko ya sera za utawala wa Rais wa Marekani kuhusu mzozo huo, siku moja baada ya Donald Trump kutangaza kusitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine.



