ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), wakiongozwa na Askofu Dk.Philemon Mollel.
Maaskofu hao na ujumbe wao wamelifika Ikulu Zanzibar kujitambulisha leo Februari 28, 2024.
Akizungumza na ujumbe huo Rais Mwinyi amesema serikali inatambua mchango unaotolewa na madhehebu ya dini zote ikiwemo kuhubiri amani na utulivu katika kuleta umoja nchini.
Aidha, Rais Mwinyi amelipongeza Kanisa hilo kwa utayari wao wa kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za kijamii nchini ikiwemo afya na elimu.
Naye Askofu Mollel amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuleta mabadiliko ya maendeleo na kuwaunganisha wananchi bila kujali itikadi za chama, kabila na dini.