Rais Mwinyi mgeni rasmi mkutano Baraza Kuu TAG

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Baraza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God(TAG), Chuo cha Biblia Miyuji, Dodoma. Tayari Rais Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea Dodoma leo.