Rais Samia afafanua uhamisho wa Maharage Chande

RAIS Samia Suluhu Hassan ametolea ufafanuzi uhamisho wa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Maharage Chande ambaye alihamishwa kutoka Shirika la Umeme (TANESCO) na kupelekea Shirika la Mawasiliano (TTCL) na jana kuteuliwa kuwa Postamasta Mkuu.

Akizungumza leo katika uapisho wa viongozi Ikulu ya Magogoni Dar es Salaam, Rais Samia amesema changamoto ya kukatika kwa umeme sio sababu ya kumuhamisha kiongozi huyo.

“Tuna changamoto kama taifa si ya mtu, mtu mwingine anaweza kusema Maharage kwa sababu ya kukatika katika kwa umeme kaondoshwa, hapana si sababu yake.”asema Rais Samia.

Rais Samia ametaja sababu inayopelekea uwepo wa changamoto ya umeme kuwa ni mitambo kwa muda mrefu haijafanyiwa huduma na kwamba itafanyiwa huduma kwa pamoja na ni lazima mitambo mingine iwake mingine izime, “kwahiyo tuna upungufu wa umeme.” Amesema Rais Samia.

Lakini pia Rais Samia ameeleza sababu ya kumtoa kiongozi huyo kutoka Shirika la Mawasiliano (TTCL) kwenda kuwa Postamasta Mkuu, kuwa ni baada ya kubaini kuwa kiongozi huyo ana biashara ndani ya shirika hilo.

“Niliona sekta ya TTCL ingekufaa zaidi … baadaye nikagundua unabiashara ndani ya TTCL na kwasababu kampuni ile inafanya vizuri nikasema hapana, usiende pahala ambapo unafanya biashara nikaona sasa nikupe Uposta Masta Mkuu,” amesema Rais Samia Suluhu wakati akiwaapisha viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x