Rais Samia alivyofanikisha mengi kwa manufaa ya taifa

1. Rais Samia ameleta shangwe kwa wahitimu wa vyuo.

Rais Samia amefuta 6% ya ada ya thamani ya mkopo ( Value Retention Fee-VRF ) kwenye marejesho yote ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) Pamoja na 10% ya faini ya kuchelewesha mikopo hiyo.
Wanufaika wote hivi sasa wanakatwa 9% tu ( single digits ) badala ya 15% waliyokatwa kabla ya Rais Samia kuingia madarakani machi 2021.

Rais Samia ameondoa kodi kwa 1% na hivyo punguzo kufikia 7% ,Hii ni sawa na kusema kiasi cha mishahara ya wahitimu hawa kimeongezeka kwa 7% mtakumbuka Rais Samia ameongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu HESLB kutoka TZS464bn mwaka 2021 mpaka TZS787.4bn.

2. Bil 400 za Mikopo ya Rais Samia kwa Wakulima yaleta tabasamu

Rais Samia Suluhu ameongeza dhamana ya mikopo jumla ya TZS355.3bn kwa wakulima sawa na ongezeko la 564% kutoka TZS63bn mwaka 2020 mpaka TZS418.3bn, Hii imesaidia wakulima wengi kukwepa mikopo ya kausha damu iliyowaacha watupu baada ya msimu wa kilimo, Ongezeko la 564% ya dhamana ya mikopo linatafsiri dhamira njema ya Rais Samia kwa ukulima na Wakulima wa Tanzania.

3. Rais Samia na Hekta Mpya 400,000 za Umwagiliaji

Bajeti ya Kilimo chini ya Rais Samia imeongezeka mara nne (4) kutoka TZS294bn hadi TZS 1.24Trilioni sawa na ongezeko la TZS946bn, Hii imesaidia ongezeko la Hekta mpya 422,083 za Kilimo cha Umwagiliaji kutoka Hekta 561,383 alizozikuta hadi jumla ya hekta 983,466. Utafiti kuhusu kilimo uliofanywa na taasisi ya Utafiti ya REPOA inasema kama Taifa tukiweza kukikuza kilimo chetu kwa 10% tutapunguza umasikini kwa 50%. Ikiwa sasa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tumekuza kilimo kwa 4.6%~5% maana yake wakati ujao tutarajie Uchumi wetu kukua.

4. Rais Samia Miaka minne (4) Megawatt 4,000

Mwaka 2021 Kenya ilikuwa inaiongoza kwa uzalishaji wa Umeme kwa nchi zote za Afrika Mashariki, Rais Samia ameongezeka uzalishaji wa Umeme kutoka 1,601.84MW mwaka 2020 hadi 4,031.71MW sawa na Ongezeko la 2,429.47MW ambazo ni sawa na ongezeko la 152%.

Hii imeongeza kiwango cha Uwekezaji wa Viwanda vikubwa na Kuifanya Tanzania sasa kuwa Wazalishaji wakuu wa Umeme EAC hata hivyo Rais Samia ndani ya Miaka minne (4) tu amepeleka Umeme kwenye Vitongoji 33,657 kati ya Vitongoji 64,359 huku vikisalia Vitongoji 30,702 tu, Hii inaleta Ulazima Kwa Watanzania kumchagua tena ili amalizie kazi hii.

5. Rais Samia hajawahi kuomba mkopo wa TZS23.3Trilioni

Pamoja na kwamba TZS2.67Trilioni , TZS11.3Trilioni na TZS9.3Trilioni zinazofanya jumla ya TZS 20.6Trilioni zinazoonekana kwenye deni la Taifa la wakati huu wa Serikali ya awamu ya Sita lakini si fedha zilizoombwa na Serikali ya awamu ya 6 kwa maelezo yafuatayo;
Kwanza, Mtakumbuka hadi kufikia Mei 2025, deni la Serikali lilifikia TZS107.70Trilion, Kati ya deni hilo, deni la nje TZS72.94Trilioni na deni la ndani ni TZS34.76 trilioni kati ya hizo jumla ya TZS11.3trilioni ikiwa ni mikopo iliyosainiwa na awamu zilizopita.

Pili, Sababu nyingine ya ongezeko la deni la nje ni kuimarika kwa dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania, Kwa mfano mwezi Machi 2021 kiwango cha kubadilisha shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani kilikuwa TZS2,298.5 wakati Machi, 2025 kilikuwa TZS2,650.

Hivyo, endapo deni la serikali litatajwa kwa shilingi ya Tanzania ni lazima lionekane limeongezeka mathalani kwa sasa deni limeongezeka kwa zaidi ya TZS9.3Trilioni.

Hatua hii ya kushuka kwa thamani kwa shilingi dhidi ya dola ya Marekani isichukuliwe kama ni hatua hasi bali ilikuwa ni hatua muhimu ya kukabiliana na mtikisiko wa uchumi wa Dunia.

Tatu, Sababu nyingine ya ongezeko la Deni la Serikali la Ndani limechangiwa na mikopo ya kugharamia miradi ya maendeleo na kulipa madeni ya ndani yaliyoiva kwa wawekezaji wa Dhamana za Serikali kwa utaratibu wa kulipia mtaji wa dhamana za Serikali zilizoiva.

Aidha, tulifanya maamuzi ya kutambua madeni mengine ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa Serikali kupitia hatifungani maalumu isiyo taslimu yenye thamani ya TZS2.67Trilioni kati ya kiasi hicho TZS2.18Trilioni madeni ya PSSSF ya waliokuwa wafanyakazi wa Serikali kabla ya 1999 (maarufu kama pre- 99).

TZS433.7bn ni madeni ya NSSF ya muda mrefu na TZS63.52bn ni madeni ya kampuni ya Ubia ya mifuko ya Pension yaani PPP (Pension Property Limited) Kampuni hii ilifadhili miradi ya Serikali kwa kutoa mikopo kwa vipindi tofauti kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya Serikali ambayo ni ujenzi wa ukumbi wa Bunge-Dodoma na ujenzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Arusha. Madeni haya hayakuwahi kuwa sehemu ya deni la Serikali

6. Utalii tiba Waongezeka mara mbili miaka minne ya Rais Samia

Katika utawala wa Rais Samia kumekua na ongezeko la utalii tiba kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hizo kutoka nje ya nchi ambapo mwaka 2020 wagonjwa kutoka nje walikua ni 5,705 na mwaka 2025 wameongezeka hadi kufikia 12,180 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 6,475 amao ni sawa na asilimia 113.

Ongezeko hili limechagizwa na ongezeko la vifaa tiba vya kisasa vya uchunguzi na ugunduzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo MRI kutoka 7 hadi 13, CT scan kutoka 13 hadi 45, Digital X-Ray kutoka 147 hadi 491 na Ultrasound kutoka 476 hadi 970,
Huduma ambazo watu walikua wanaenda kuzipata nje ya nchi kwa sasa zinapatikana nchini. Uboreshaji wa huduma mbalimbali ikiwemo ongezeko la Idadi ya hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa ya dharura (EMD) imeongezeka kutoka hospitali saba (7) mwaka 2020 hadi 125 mwaka 2024, Ongezeko la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba aina 382 katika vituo vya umma kutoka asilimia 73 mwaka 2020 na kufikia asilimia 86.2 Aprili, ongezeko la Idadi ya vitanda kutoka 84,162 mwaka 2020 mpaka kufikia vitanda 123,769 mwaka 2024.
7. Tanzania ya pili Ukanda wa EAC mapambano dhidi ya Rushwa,
Juhudi zilizofanywa na Rais Samia katika kupambana na rushwa zimeiwezesha Tanzania kushika nafasi ya pili katika Ukanda wa Afrika Mashariki na nafasi ya 14 kwa nchi za Afrika kwenye mapambano dhidi ya rushwa, kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya Transparency International ya mwaka 2024, sambamba na mafanikio haya ni katika kipindi hiki ambapo serikali anayoingoza iliongoza nguvu kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ambapo ilifanya oparesheni mbalimbali na kufanya uchunguzi wa wa tuhuma za rushwa.Jitihada hizo zilisaidia kuthibiti na kuokoa kiasi cha TZS211.95bn Aidha, mali zenye thamani ya TZS35.688bn zikijumuisha nyumba, viwanja, magari na fedha taslimu TZS1.17bn zilitaifishwa na serikali.
8. Huduma za Afya Tanzania sasa ni kilometa 5 tu.
Rais Samia ameongeza bajeti ya Wizara afya kutoka TZS900bn mwaka 2020/21 hadi TZS1.618Trilioni mwaka 2025 sawa na ongezeko la TZS 718bn, Ongezeko hili limepelekea kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 8,783 mwaka 2020 hadi 12,846 mwaka 2025 sawa na ongezeko la vituo vipya 4,063, ambapo 75% ya wananchi wanapata huduma za afya ndani ya km 5 ya maeneo wanayoishi,

9. Wakati Rais Samia anaingia madarakani kulikuwa na malalamiko mengi ya wafanyakazi kuhusu Kikokotoo,
Kwanza, Mwaka 2020 Unufaika wa malipo ya mkupuo wa asilimia 50 Ulishushwa hadi 33%, Hata hivyo mwaka 2025 Rais Samia ameuongeza unufaika huo mpaka 40%.
Pili, Mwaka 2020 unufaika wa asilimia 25 nao ulipunguzwa kwa 33%, Hata hivyo mwaka 2025 Rais Samia ameuongeza hadi 35%.
Hii imeongeza Ari,Nguvu na imani ya Wafanyakazi kwa Serikali yao chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
10. Rais Samia aongeza mapambano dhidi ya dawa za kulevya
Vituo vya utoaji huduma za tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya
vyaongezeka mara mbili katika miaka minne ya Rais Samia.
Rais Samia ameongeza vituo vya utoaji huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya kutoka vituo 9 mwaka 2020 hadi 18 mwaka 2020. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 50 ya vituo hivo ambapo miongoni mwa huduma zinazotolewa ni pamoja na tiba ya methadone,ushauri nasaha na huduma za afya ya akili, elimu ya Ukimwi na upimaji wa VVU, kupatiwa elimu ya kinga kupima na kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Kifua kikuu na Magonjwa ya zinaa, pia Kupatiwa Elimu juu ya maambukizi ya Homa ya ini B na C.
Serikali pia imeimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kupunguza uingizaji, uzalishaji na usambazaji wa dawa za kulevya kwa kubaini na kudhoofisha mitandao ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya. Ambapo katika kipindi hiki, Kilogramu 4,697,511.35 za dawa za kulevya zimekamatwa ambapo zimehusisha watuhumiwa 25,715.

11. Uwekezaji wa $1 kwenye Elimu huzalisha $5 kwenye GDP kwa mwaka (UNESCO).

Mwaka 2021 wakati Rais Samia Suluhu anaingia madarakani bajeti ya Elimu ilikuwa TZS4.72Trilioni ameiongeza hadi TZS6.16Trilioni 2024/25. Ongezeko ni TZS1.44Trilion sawa na 31% UNESCO wanasema kila $1 kwenye Elimu inazalisha $5 kwenye GDP ndio sababu ya Uwekezaji huu mkubwa.

UNESCO wanasema nchi kama Tanzania ikiwekeza kwenye Elimu kiasi cha dolla moja ya kimarekani itazalisha kwenye Uchumi jumla ya $5 kwa kila mwaka.

Kama Tanzania tumekeza kiasi cha $2.4bn ikizidisha na $5 utapata jumla ya $12bn kwa mwaka hii ni sababu moja wapo ya Rais Samia kuongeza kiasi kikubwa cha bajeti kwenye sekta hii ya Elimu nchini.

12. Rais Samia aondoa migogoro ya Ardhi
Rais Samia tangu aingie madarakani mwaka 2021, amechukua juhudi mbalimbali katika kutatua migogoro ya ardhi ambapo serikali kupitia wizara ya ardhi zilichukua hatua za mpango wa usuluhishi wa migogoro kwa kupunguza ucheleweshaji wa mashauri kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kiutawala,juhudi hizi zimewesha kufanikisha utatuzi wa migogoro 8,633 kati ya 11,860 kati ya mwaka 2021 hadi 2024 sawa na asilimia 73.2 ya migogoro yote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button