Rais Samia amfuta kazi Katibu Mkuu Wizara ya Maji
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba kuanzia leo Agosti 18, taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema.
Kemikimba aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu mwezi Februari 2023, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu. Pia ametumikia nafasi mbalimbali ikiwamo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Maji.
Pamoja na hilo, Mhandisi Kemikimba amefanya kazi katika Idara ya Huduma za Ubora wa Maji kuanzia ngazi za kiufundi mpaka uongozi wa idara inayosimamia masuala ya ubora wa maji Wizarani.