Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga Vs USM Algers

Rais Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amenunua tiketi 5000 kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Yanga na USM Algers utakaopigwa Mei 28, 2023 Dimba la Mkapa, Dar es Salaam.

Akiwasilisha ahadi hiyo ya Rais Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema lengo la Rais Samia ni kutengeneza mazingira mazuri kwa Yanga kutwaa ubingwa wa huo na kuandika historia mpya kwenye soka la Tanzania.

Aidha Msigwa amesema Rais Samia amewataka wadau wengine kujitokeza kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo ili kuwapa nafasi mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo na Yanga kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa nguvu ya mashabiki.

Advertisement

Yanga wamekuja na kauli mbiu maalumu kuelekea kwenye mchezo huo wa fainali ijulikanayo kama WHY NOT US ( kwanini sio sisi)

1 comments

Comments are closed.