Rais Samia apongezwa kuteua mpinzani

WADAU wa siasa na wananchi wamewatwika mzigo wa majukumu viongozi wapya walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakiwataka watekeleze majukumu yao kwa weledi, uadilifu na kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya binafsi. Wakizungumza na HabariLEO jijini Dar es Salaam, wadau hao wamesema uteuzi huo unaweka matarajio makubwa kwa viongozi hao, hivyo wanapaswa kuonesha utendaji wenye tija na uwajibikaji kwa wananchi.

Pamoja na wito huo, wamempongeza Rais Samia kwa kile walichokiita ukomavu wa kisiasa katika kufanya uteuzi huo, hususani kumteua Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Dk Eveline Munisi kuwa mbunge na Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu).

Mdau wa siasa, Handhal Al Khaify alisema Profesa Kabudi ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa na mwenye uwezo wa kuhimili majukumu ya wizara hiyo yenye uzito mkubwa. “Ni uteuzi sahihi, ana uzoefu wa kutosha na naamini ataweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,” alisema Al Khaify.SOMA: Lukuvi ampongeza Rais Samia uteuzi wa Mwigulu

Dorotea Mtandu amesema anaamini Profesa Kabudi ataendeleza na kuboresha kazi iliyofanywa na mtangulizi wake, William Lukuvi aliyefariki dunia Machi 25, mwaka huu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kutokana na maradhi ya mshituko wa moyo.

“Tunamtakia kila la heri na tunatarajia atafanya kazi kwa bidii na uwajibikaji,” alisema Mtandu. Mkazi wa Dar es Salaam, Cadillac Frank alisema Rais Samia amefanya uamuzi sahihi kwa kumteua Profesa Kabudi, akieleza kuwa ni kiongozi mwenye misimamo na uwezo wa kusimamia majukumu ya serikali. “Huu ni uteuzi mzuri, ana uzoefu na amewahi kufanya vizuri katika wizara nyingine,” alisema Frank. Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba alimpongeza Profesa Kabudi kwa kuaminiwa na Rais Samia.

Kwa upande wake, Profesa Kabudi akimshukuru Rais Samia kwa imani hiyo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii. “Ninamshukuru rais kwa kuniamini, nitafanya kazi kwa juhudi na uaminifu mkubwa katika kulitumikia taifa,” alisema Profesa Kabudi. Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Haji Khamis amesema  uteuzi wa Dk Munisi unaashiria kukua kwa demokrasia nchini na kuimarika kwa siasa jumuishi.

Amesema hatua hiyo inaonesha kuwa serikali inatambua uwezo wa viongozi kutoka vyama mbalimbali vya siasa na kuwapa nafasi ya kuchangia maendeleo ya taifa. “Ni ishara nzuri ya kisiasa, inaonesha kuwa siasa si uadui, bali ni ushindani wa mawazo kwa ajili ya maendeleo ya nchi,” alisema Khamis. Ameongeza kuwa kwa uzoefu wake wa kufanya kazi na Dk Munisi, amebaini kuwa ni kiongozi mwenye sifa za uongozi, ikiwemo weledi, hekima, busara na uzalendo.

Wakati huo huo, Taasisi ya Women in Leadership Forum (WLF) imempongeza Mwenyekiti wake, Dk Munisi kwa kuteuliwa kuwa mbunge. Kupitia taarifa yake, taasisi hiyo imesema uteuzi huo ni heshima kubwa si kwa Dk Munisi pekee, bali pia kwa wanawake wote wanaoamini katika uongozi wenye maono na dhamira ya kulitumikia taifa. “Tunaamini huu ni uthibitisho kuwa mchango wa wanawake unaendelea kutambuliwa katika ngazi za juu za maamuzi,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, taasisi hiyo ilieleza kuwa ina imani Dk Munisi ataendelea kulitumikia taifa kwa hekima, weledi na uadilifu. Katika uteuzi huo wa hivi karibuni, Rais Samia pia aliteua viongozi wengine ambao ni Katibu wa Rais Ikulu, Balozi Ali Jabir Mwadini na kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Ewura, Dk James Andilile Mwainyekule.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Start now generating extra home based cash by doing very easy and simple job from home. Last month i have earned $19753 from this job in my part time. This job is just awesome and its earning are greater than 9 to 5 office job. Join this right now by follow instructions here…

    >>>>>>>>>> http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button