Rais Samia arejesha amani ya nchi

DAR- ES-SALAAM : WAZIRI Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba amesema serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imefanikisha kurejesha utulivu wa kisiasa nchini, baada ya kipindi kigumu cha miaka mitatu ambapo uhuru wa wanasiasa ulidhibitiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisisitiza kuwa hatua hiyo imeweza kuifanya nchi kuwa katika hali ya utulivu, ingawa baadhi ya wanasiasa sasa wanajaribu kutaka kuharibu amani ya nchi.

“Miaka mitatu iliyopita hali ya siasa haikuwa nzuri  ikiwemo mivutano ya siasa, maandamano  yalizuiliwa, na hata uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa shida,” alisema Warioba.

Advertisement

Aliongeza, “Katika kipindi hiki , tumeweza kuongoza nchi na sasa imetulia.”

Jaji Warioba  amesema viongozi wa serikali na vyama vya siasa wanapaswa  kutambua dhamana zao  kwa wananchi kuendelea kulinda amani ya nchi.

SOMA :  Afrika rejesheni amani Sudan