Rais Samia ataja mbinu za kutokomeza Malaria Afrika

ETHIOPIA: RAIS Samia Suluhu Hassan amesema mapambano dhidi ya malaria barani Afrika yanahitaji uongozi na usimamizi thabiti wa Waafrika wenyewe, umiliki wa kweli wa programu zake na dhamira ya kisiasa ya muda mrefu.

Rais Samia alisema hayo jana aliposhiriki katika mkutano wa ngazi ya juu na vyombo vya habari uliolenga kujadili ufadhili endelevu wa mapambano dhidi ya Malaria barani Afrika, mbali na Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huo ulioandaliwa na AU kwa kushirikiana na Umoja wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria (ALMA), ulilenga kujadili namna
ya kuimarisha ufadhili wa ndani wa programu za malaria, kupunguza utegemezi wa misaada ya nje pamoja na kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika.

Alisema vita dhidi ya malaria si suala la afya pekee, bali ni ajenda ya maendeleo, uchumi na ustawi wa rasilimali watu Afrika.

Akieleza uzoefu wa nchi katika mapambano dhidi ya malaria, alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika ajenda ya kutokomeza malaria, ikiwa ni pamoja na kuwa mwenyeji wa ALMA kama taasisi ya kuratibu mapambano hayo barani Afrika, iliyojengwa juu ya mifumo madhubuti ya uwajibikaji pamoja na uwezo
wa utekelezaji unaolenga matokeo.

Aidha, alisema Tanza- nia imewekeza kwa kiasi kikubwa katika tafiti za kisayansi na ubunifu kupitia Taasisi ya Afya Ifakara (IHI), ikiwemo utafiti wa teknolojia za kisasa za kudhibiti maambukizi ya malaria.

Kadhalika, alibainisha jitihada za Tanzania za kuongeza matumizi ya vyandarua vya kujikinga dhidi ya mbu waenezao malaria, chanjo za malaria pamoja na kuboresha mifumo ya matibabu na ufuatiliaji wa wagonjwa.

Aliongeza kuwa, serikali imeimarisha ushirikiano wa sekta mbalimbali ili
kuhakikisha afua za malaria zinaunganishwa kikamilifu katika mfumo wa huduma za afya ya msingi na Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma na kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.

Katika kuimarisha ufadhili wa ndani, Rais Samia alisema kupitia Mabaraza ya Kutokomeza Malaria ya Tanzania Bara na Zanzibar, serikali imeendelea kush- irikiana na sekta binafsi, taasisi za dini, asasi za kiraia na wadau wa maendeleo kwenye uhamasishaji wa rasilimali za ndani kwa ajili ya mapambano dhidi ya malaria.

Kwa upande mwingine, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa, akieleza kuwa pamoja na jitihada za ndani, taasisi
za kimataifa na washirika wa maendeleo wanapaswa kutekeleza ahadi zao kikamilifu na kwa wakati, hususan katika kuimarisha Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Malaria na matumizi ya rasilimali za Benki ya Dunia kwa ajili ya programu za Malaria.

Vilevile, Rais Samia alisema jitihada za kuto- komeza malaria zinahitaji mshikamano wa pamoja wa nchi wanachama, ufadhili endelevu na matumizi ya takwimu sahihi katika kufanya maamuzi pamoja na ubunifu unaozingatia mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, Rais wa Botswana na Mwenyeki- ti wa ALMA, Duma Gideon Boko, alidokeza kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Malaria barani Afrika ya mwaka 2025, Afrika bado ipo mbali kufikia lengo la kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030.

Rais Boko alihimiza nchi wanachama kutenga bajeti mahsusi kwa ajili ya mapambano dhidi ya malaria, kuanzisha Mabaraza ya Kutokomeza Malaria pamoja na kutumia mifumo ya takwimu ili kuboresha utekelezaji.

Naye, Kamishna wa Afya, Masuala ya Binadamu na Maendeleo ya Jamii wa Umoja wa Afrika, Balozi Amma Twum Amoah alisema kupungua kwa ufadhili wa kimataifa katika miaka ya karibuni kumeathiri juhudi za nchi mbalimbali za kupambana na malaria.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  www.join.work27.com 

  2. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  3. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button