Rais Samia ataka mifumo bora usimamizi fedha

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wahasibu wakuu wa nchi za Afrika kujenga  imani ya wananchi katika mifumo ya usimamizi wa fedha za umma ili kuhakikisha fedha za hizo zinatumika kwa ufanisi, uwazi ikiwemo kuweka mifumo imara ya kudhibiti mianya ya rushwa

Pia amewataka kubuni  mbinu mpya za usimamizi wa fedha za umma, kupitia matumizi ya teknolojia ya kidijitali, ili kuongeza  uwajibikaji kuboresha ufanisi na uwazi wa matumizi ya fedha za umma itasaidia katika kupunguza rushwa na kuongeza uaminifu wa umma katika mifumo ya kifedha.

Advertisement

Maagizo hayo yametolewa leo jijini Arusha na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa  niaba ya Rais ,Samia wakati akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (AAAG) wenye kauli mbinu ya “Kujenga Imani ya Umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu.”

Amesema  wahasibu wakuu wa serikali wanajukumu la kuongoza mageuzi katika mifumo ya kifedha ambayo yatachochea ukuaji endelevu, kupunguza umaskini, na kuhakikisha kwamba rasilimali zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi.

Naye Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA, Leonard Mkude amesisitiza mkutano huo wa siku tatu utajadili mambo mbalimbali ikiwemo usimamizi mzuri wa mifumo  ya fedha ikiwemo kuweka mifumo dhabiti ya kudhibiti mianya ya rushwa na upotevu wa fedha za umma sanjari na matumizi ya teknolojia katika masuala ya fedha.