Rais Samia atoa zawadi kwa wazee na watoto Tanga

RAIS wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi za sikukuu zenye thamani ya Shilingi milioni 11.3 katika vituo 15 vya wazee na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu mkoani Tanga.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Samia ,Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba amesema kuwa zawadi hizo zimelenga katika kusherehekea sikuuu ya Christmas na mwaka mpya.

Amesema kuwa wakati huu ambao Wananchi wengi wapo katika maandalizi mbalimbali Kwa ajili ya kusherehekea siku hivyo Rais ameona ipo haja ya kuwakumbuka makundi ya watu wenye uhitaji Ili nao waweze kufurahia siku hiyo.

“Zawadi hizo zimetolewa katika vituo vilivyoko kwenye wilaya za Tanga, Handeni,Kilindi,Muheza na Pangani kwa watoto na wazee ambao wanalelewa katika vituo Ili nao waweze kusherehekea vizuri sikukuu hiyo”amesema Rc Mgumba.

Nae Mzee anaelelewa katika kituo Cha wazee cha Mwanzange jijini Tanga Isdory Dismas amemshukuru Rais Samia Kwa zawadi hizo na kumuombea Kwa mungu aendelee kumlinda na ,kumuongoza katika uongozi wake.

“Tupelekee salamu zetu sisi wazee tunamuombea kwa mungu katika vipindi vya utawala wake mungu akulinde Ili uweze kuendelea kutufanyia yaliyo mazuri zaidi”amesema Dismas .

Habari Zifananazo

Back to top button