Rais Samia azindua safari za SGR

DAR-ES-SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi treni ya kisasa ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika stesheni kuu ya Dar es Salaam, zikiwa na lengo la kuboresha miundombinu na usafiri nchini Tanzania.

Treni hii mpya itarahisisha safari kati ya miji hiyo miwili muhimu, ikipunguza muda wa safari na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo.

Advertisement

SOMA: LATRA yatangaza bei Daraja la Kawaida SGR

Uzinduzi huu unatarajiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Tanzania.