RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan asubuhi hii anatarajiwa kuzindua rasmi usafiri wa treni ya umeme katika reli ya kisasa (SGR ya Shirika la Reli Tanzania(TRC) kwa kusafiri kwa treni hiykutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
SOMA: Rais Dk. Mwinyi kushiriki Uzinduzi wa SGR
Reli ya SGR Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma yenye urefu wa kilometa 722, ni sehemu ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi wa SGR kuelekea mikoa ya Magharibi na Kanda ya Ziwa.
Safari ya kutoka DAR-MOROGORO hutumia saa moja na dk 45 huku kutokea DSM hadi DODOMA ikitumia saa tatu na dk 25, huku ikiwa na uwezo wa kubeba tani 10 za mizigo sawa na malori 500.