Rais Samia mgeni rasmi mkutano viongozi taasisi za serikali

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua kikao kazi cha Wenyeviti na Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali, utakaofanyika Jijini Arusha kesho Agosti 19, 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema hayo leo Agosti 18, 2023 alipotoa taarifa ya maandalizi ya kikao hicho na kusema mbali na Rais, viongozi wengine watakaokuwepo ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson na mawaziri mbalimbali wa Baraza la Mawaziri.

Alisema Samia pia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye madhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la kiluthelu Nchini, KKKT yatakayofanyika kwenye Chuo cha Makumira, Arumeru.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Mashirika ya Umma  na Taasisi za Serikali Sabasaba Moshingi amesema hicho ni kikao kazi cha kwanza kufanyika lengo la kikao hicho ni kuziwezesha taasisi na mashirika kutengeneza faida na kutoa huduma bora na nzuri.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akiongea na waandishi wa habari Jijini Arusha leo juu ya ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma.

Amesema kuwa Jumla ya taasisi 248 yakiwemo mashirika ya umma na taasisi za serikali yatashiriki kikao hicho ambapo wajumbe zaidi ya 1000 watakuwepo .

Amesema kuwa kauli mbiu ya kikao hicho ni mwelekeo mpya wa usimizi na uendeshaji wa taasisi za umma.

Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa, AICC, Balozi mstaafu Ephraimu Mafuru amesema Tanzania iko katika yetu nafasi ya  tano barani Afrika kwa kuandaa mikutano ya utalii kimataifa.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali, Sabasaba Moshingi (kulia ) akizungumza na waandishi wa habari

Amesema nchi ambazo zimeitangulia Tanzania katika Afrika ni pamoja na Afrika kusini, Moroco, Rwanda na Misri,na bado nchi inaendelea kufanya vizuri kwenye uchumi.

Amesema kuwa nchi ni mwanachama wa Taasisi ya ICA, ambayo ni taasisi inayoandaa mikutano mikubwa inayofanyika  Afrika na kila mwaka AICC inapokea taarifa kutoka kwenye taasisi hiyo imefikia nafasi ya ngapi Katika kuandaa mikutano ya uchumi wa utalii.

Amesema mwaka 2019  Katika mikutano iliyofanyika Afrika Tanzania iliandaa mikutano 19 ambayo ni sawa na asilimia 30% ya mikutano yote inayoaandaliwa na taasisi hiyo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Balozi Mtaafu Elpherem Mafuru akitete na baadhi wa washiriki wa mkutano huo

Ameongeza kuwa mwaka 2022 nchi yetu ilifanikiwa kuandaa mikutano 18 iliyofanyika barani Afrika na mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Rais Samia ya kufungua nchi na tupo kwenye uchumi wa mikutano.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la viongozi mashirika ya umma na taasisi za serikali ,Latifa Mohamed Hamisi amesema kuwa wanatarajia kupata mwelekeo mpya wa usimamizi wa mashirika ya umma na taasisi za serikali katika kutoa huduma bora na baada ya kikao hicho kutakuwa na mabadiliko ya utendaji.

 

Habari Zifananazo

Back to top button