RAIS Samia Suluhu Hassan amesema angependa Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu ya Zanzibar kuandaa mkutano wa viongozi wa serikali kwa ajili ya kukumbusha namna ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utendaji kazi.
Rais Samia amesema hayo alipofanya mkutano wa faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha leo Machi, 02 2023.
“Katika mkutano huu kuna Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, pengine atakapotoka hapa naye kwake atakwenda kufanya hivyo, nasisi tupo tayari kuja na kuwasaidia.”amesema Rais Samia.