Rais Samia ni alama ya matumaini – Majaliwa

DODOMA: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa akimnukuu Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kama mwanasiasa maarufu zaidi nchini Tanzania, akimueleza kama mwalimu wa subira, kielelezo cha ujasiri na alama ya matumaini.

Majaliwa ameyaeleza hayo katika hotuba yake kwa Bunge la Tanzania, wakati akihitimisha mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge ambalo limeongozwa na maspika wawili, Job Ndugai na Dk Tulia Ackson.

“Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa nwalimu wa subira, Kielelezo cha ujasiri, Ustahimilivu na alama ya matumaini kwa kizazi hiki na kijacho. Ninaomba nimnukuu Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alisema hapa Tanzania leo hakuna mwanasiaza maarufu kama Rais Samia iwe ndani ya Chama au nje ya CCM” amesema Majaliwa.

Majaliwa atoa maagizo 7 kwa taasisi, watumishi wa umma

 

Majaliwa amebainisha kuwa katika kipindi cha uongozi imara na wenye hekima wa Rais Samia, Tanzania imeendelea kusimama imara, kusimamia tunu za taifa za amani na utulivu, kuendeleza miradi ya maendeleo ya Kimkakati na huduma za kijamii, kuimarisha demokrasia pamoja na kuimarisha diplomasia, kujenga uchumi na mshikamano wa Kitaifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button