Rais wa AfDB anayemaliza muda wake atembelea nchini

RAIS wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dk Akinwumi Adesina amewasili jijini Dar Es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku 4 kuanzia leo hadi Juni 15.

Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam amepokewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Denis Londo.

Wakati wa ziara hiyo, Dk Adesina anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Dk Adesina na Rais Samia watashiriki hafla ya ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na barabara ya mzunguko jijini Dodoma Juni 14, 2025.

Katika ziara hiyo, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kitamtunukia Shahada ya Heshima ya Falsafa Dk Adesina Juni 13.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button