Ruto awateua wapinzani uwaziri

KENYA: Rais wa Kenya, William Ruto amewateua baadhi ya viongozi wa upinzani katika baraza lake la mawaziri .na pia amerejesha mawaziri wa zamani wanne waliokuwa katika baraza lake la hapo awali ,akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Sheria Justin Muturi ambaye sasa ni miongoni mwa waziri walioteuliwa.
Mawaziri hao ni John Mbadi amekuwa Waziri wa Fedha,Salim Mvurya ameteuliwa kuwa Waziri wa Uwekezaji, Rebecca Miano ni Waziri wa Utalii, Opiyo Wandayi –Kawi Kipchumba Murkomen amechaguliwa kuwa Waziri wa Vijana na Michezo.
Wengine Hassan Joho amepelekwa Madini na Alfred Mutua ni Waziri wa Kazi na Wycliffe Oparanya wa Vyama vya Ushirika huku Justin Muturi akiteuliwa kuwa Waziri wa Utumishi wa Umma na Stella Langat kawa Waziri wa Jinsia.
SOMA: Ruto Atangaza Baraza Jipya la Mawaziri