KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini aliyesimamishwa kazi, Yoon Suk Yeol, amejitokeza kwa mara ya kwanza katika kesi ya kuondolewa madarakani, ambapo amekanusha tuhuma za kuamuru kukamatwa kwa wabunge wakati wa jaribio lake la kutunga sheria ya kijeshi.
Bunge lilipiga kura ya kutokuwa na imani na Yoon mwezi uliopita, na mahakama ya kikatiba iliamua kumkamata na kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Wakati wa kusikiliza kesi hiyo, Yoon alikanusha kutoa amri kwa makamanda wa kijeshi kuwakamata wabunge waliokataa kutekeleza sheria ya kijeshi aliyokuwa amepanga kuitangaza.
“Mimi ni mtu ambaye nimeishi kwa imani thabiti katika demokrasia huria,” alisema Yoon, akisisitiza kuwa sheria hiyo haikupangwa kutekelezwa.
SOMA: Hatimaye Rais Yoon Suk akamatwa