RC apiga marufuku uuzaji ardhi holela Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amepiga marufuku uuzwaji holela wa maeneo yenye migogoro ya ardhi

Huku akiwataka wakuu wa wilaya kuwa chukulia hatua kali za kisheria viongozi wa vijiji na kata ambao wanaohusika kuuza ardhi bila ya kufuata utaratibu uliopo.

Agizo hilo amelitoa leo wakati akikagua eneo la mpaka kati ya kijiji cha Gitu kilichopo wilayani Kilindi na Ngobole wilayani simanjiro ambalo limekuwa na changamoto ya mgogoro baina ya wakulima na wafugaji.

“Kiongozi Yeyote ambaye atathibitika Kwa makusudi kuuza Kwa mara ya pili maeneo ambayo yanamigogoro ya ardhi hatutamuonea haya awe Kiongozi wa Serikali au Chama lazima tutakomaa nae”amesema RC Kindamba.

Natusi Manumbu, Afisa Ardhi Wilaya ya Kilindi amesema kuwa muingiliano wa maeneo umekuwa ukichangia kuzalisha migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika eneo hilo.

Amesema licha ya maeneo ya kilimo na malisho kutengwa lakini kumekuwa na mwingiliano wa maeneo kutokuwa na viongozi kukuza ardhi kiholela.

Habari Zifananazo

Back to top button